April 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

STAMICO na NMB wakubaliana kuwainua kiuchumi wachimbaji wadogo

Na David John

SHIRIKA la Madini la Taifa Stamico na Taasisi ya Kifedha ya Benki ya NMB wametiliana saini ya mashirikiano na makubaliano kwa lengo la kuwainua wachimbaji wadogo kupitia sekta ya madini kuwapatia mikopo.

Tukio hilo la kusaini makubaliano hayo yamefanyika katika ofisi za makao makuu ya shirika la Madini nchini Stamico ambapo shirika limesema huo uendelezaji wa mkakati wa shirika la Stamico ili kwenda kumshika mkono mchimbaji mdogo.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Stamico Dkt Venance Mwasi amesema hadi kufikia sasa wao kama shirika wameshatoa leseni elfu 34 kwa wachimbaji wadogo ambao ni wazawa hapa nnchini.

Ameongeza kuwa ili kuchochea ukuaji wa uchumi na wachimbaji wadogo kupata faida na ndio maana leo wanafikia makubaliano na Nmb ili iweze kutoa fursa ya kukopesha wachimbaji hao na hata wao kama taasisi wannapenda kupata wateja ili fedha iweze kuzunguka.

Dkt. mwasi amefafanua kuwa madini kama haya chimbwi kunakuwa hakuna maana yeyote hivyo amewaomba Nmb kutoa fursa ya mikopo kwa wachimbaji hao wadogo.

“Makubaliano haya yanakwenda kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwa wachimbaji na yanakwenda kunufaisha wote wawili kwa maana ya benki na wachimbaji hawa ambao ni wateja.” Amesema

Ameongeza kuwa muafaka huo unakwenda kutengeneza ukuaji wa kodi na kubwa zaidi kutakuwa na mzunguko mkubwa wa fedha na shirika linakwenda kunufaisha wachimbaji wadogo huku akiwataka wachimbaji hao kubadilika na kufuata sheria.

Mkurugenzi huyo alisema biashara ni ushindani na hivyo kitendo cha kuingia makubaliano na taasisi za fedha ni mpango kababe ambao lengo lake hasa ni kutaka kuwasaidia wachimbaji wadogo na ndio maana siku chache zilizopita walikubaliana na GST kwa maana wao ndio watalaamu ambao wanajua wapi mahala ambapo pana madini.

Amesema wao kama Stamico wamenunua mashine tano kwa ajili ya kuchoronga madini na mashine hizo ndio mwarobaini na wakishachoronga wanakwenda kupima na kupata uhakika wa uwepo wa madini katika eneo husika .

Amesema huo ni mwazo na wataendelea kununua mashine kwa ajili ya wachimbaji wadogo na huko nyuma mchimbaji mdogo ilikuwa kama shida hivyo wameamua kuwashika mkono na wanatarajia kuleta muwekezaji kutoka nje ya nchi ambayo atakuja pia kusaidia wachimbaji hao wadogo.

Kwaupande wake Afisa Mkuu wa Mikopo kutoka Nmb Daniel Mboto .aliwashukuru stamico kwa kukubaliana kuwa pamoja katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wananufaika na nmb.

Amesema NMB kwao ni mwendelezo kwani hata wao wapo kwenye maeneo mbalimbali ya migodi na ushirikiano huo ndio umefikia leo kuingia kwa mara nyingine na stamico kwa ajili ya wachimbaji wadogo.

Amesema taasisi za fedha zipo kwa ajili yo na amewataka kujitokeza kwa mameneja wa mikopo ili kupata taarifa zao ambazo zitawawezesha kupata fedha au mikopo kupitia Nmb.

Ameongeza kuwa kwaupande wa shirika la madini ni kuwa na taarifa sahihi za mchimbaji huyo ili hata atakapokuja kwao kwa ajili ya mikopo aweze kuaminika na kupata mkopo kwa ajili ya shughuli zao za uchimbaji .

“Nawashukuru sana stamico kwa kufikia makubaliana haya ambayo yanakwenda kuwa na tija katika nchi na kwa wachimbaji hawa wadogo.” amesema

Alisema wao kama NMB wanamikakati ya muda mrefu na mfupi na waliweka milioni 123 na hivi sasa wameshatoa mikopo hadi milioni 20 na kwa makubaliano hayo wataendelea kasi ya kukopesha.

Kuhusi mikopo alisema mkopo kwa kutumia wadau wao ambao ni Stamico ,benki itatoa mikopo rafiki kwa wachimbaji na wadau mbalimbali wa sekta ya madini .

Alisema pia watatoa elimu ya fedha kwa wadau katika sekta ya madini ili kusaidia katika kuhakikisha matumizi sahihi ya fesha yanafanyika.

“Nifursa ya kipekee sana kwa wachimbaji wadogo na wadau wa sekta ya madini kwani kwa kila hatua ya shughuli zao ,benki ya Nmb na Stamico tuko nao kuhakikisha wanafanikiwa.” alisema

Amefafanua kiwa mteja anapata muongozo wa namna ya kuwekeza na wapi pakuwekeza kutoka Stamico ,baadae benki ya Nmb inampa mkopo rafiki kabisa wakati mteja anaendelea na shughuli zake.

“Nitoe rai kwa wadau wa sekta ya madini kuchangamkia fursa hii na watembelee matawi ya Nmb kwa ajili ya maelekezo ya mikopo ambayo kwa sasa itakuwa na baraka na miongozo kutoka Stamico na kuwafanya wapige hatua mbele zaidi katika biashara na shughuli zao.” amesema

Kwa upande wake mwakilishi wa wachimbaji wadogo Salma kundi kutoka TAWOMA aliwashukuru Stamico na kwamba kwao ni siku ya kihistoria na kwaniaba ya wachimbaji wadogo wote amesema wao watajitahidi kwakufuata utaratibu wote ili waweze kunufaika.

Afisa Mkuu Mikopo kutoka NMB Daniel Mbotto (kushoto) akibadilishana mikataba ya makubaliano na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Madini la Taifa Stamico Dkt Evance Mwasi.hafla iliyofanyika ofisi za stamico

Afisa Mkuu mikopo NMB Daniel Mbotto (kushoto) akisaini karatasi ya makubaliano na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Stamico Dkt.Evance Mwasi naye akisaini.
Kaimu Mkurugenzi Stamico Dkt Evance Mwasi (kulia) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani kushoto ni Afisa Mkuu mikopo Daniel Mbotto .