April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia akabidhi Pikipiki 26 kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani leo tarehe 23 Novemba 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu matumizi ya Barabara alipotembelea mabanda ya maonesho kwenye maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yaliyofanyika leo tarehe 23 Novemba 2021 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.Wa pili kulia Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu matumizi ya Barabara na Madaraja pamoja na kuvuka katika maeneo hayo  kutoa kwa Watoto wa Shule mbalimbali mkoani  Arusha alipotembelea mabanda ya maonesho kwenye maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika leo tarehe 23 Novemba 2021 katika Uwanja wa  Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. wa pili kulia Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akikabidhi jumla ya Pikipiki 26 kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro kwa ajili ya kuongeza kasi ya kufanya Doria kwa Jeshi hilo, kwenye maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yalioanza leo tarehe 23 Novemba 2021 katika Uwanja wa  Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.  Khamis Hamza Chillo