October 20, 2021

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Shule za St Mary’s zaendelea kuwa juu kitaaluma

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira,Online, Dar

SHULE za St Mary’s zimepongezwa kwa mafanikio mazuri ya kitaaluma na kwa namna ambavyo imewalea wanafunzi katika maadili mema.

Pongezi hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Shule Kuu ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUCE), Eugenia Kafanabo, kwenye mahafali ya 20 ya shule ya sekondari St. Marys Mbezi.

Amesema shule hizo zimefanikiwa kujenga heshima kwa kuzalisha wanafunzi wenye nidhamu na uwezo mkubwa kimasomo kutokana na kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi kujisomea.

Wahitimu wa kiume wa kidato cha nne wa shule ya St Mary’s Mbezi jijini Dar es Salaam wakiingia kwenye mahafali hayo ya 20 kwa mbwembwe mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Shule Kuu ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUCE), Eugenia Kafanabo.

“St Mary’s ni miongoni mwa shule kongwe na bora nchini kwa kuwa na walimu mahiri na wa kutosha. Haya ni mahafali ya 20 hivyo uzoefu huu unaipa shule nafasi kubwa ya wanafunzi wake kufanya vizuri zaidi na waingereza wanasema Experience is the best teacher,” amesema Kafanabo

Aidha, amesema mbali na mafanikio ambao nchi imeyapata bado kuna changamoto ya upungufu wa wataalamu katika sekta ya afya na masuala yanayohusu sayansi na teknolojia hivyo aliwataka kuchangamkia masomo hayo.

Mkuu wa Shule Kuu ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUCE), Eugenia Kafanabo, akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya sekondri ya St Mary’s Mbezi kwenye mahafali ya 20 ya shule ya sekondari hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shule hapo.

“Kuna changamoto zinazohitaji wasomu wabobezi kuzitatua hivyo nawashauri kufikiria kujiunga na ngazi ya elimu ya juu na kwa bidii masomo ya sayansi kwani hiyo ndiyo njia pekee ya taifa letu kupata hazina ya rasilimali watu itakayoweza kupiga hatua kwenye maendeleo,” amesema

Amesema mbali na mchango kwa taifa elimu bora inafungua njia za maisha binafsi pamoja na familia kwani watanzania wengi wamezaliwa vijijini ambako wazazi walipata changamoto nyingi za kuwasiadia watoto wao kusoma.

Wahitimu wa kike wa kidato cha nne wa shule ya St Mary’s Mbezi jijini Dar es Salaam wakiingia kwenye mahafali hayo ya 20 kwa mbwembwe mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Shule Kuu ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUCE), Eugenia Kafanabo.

“Wazazi na walezi wetu walifikia hatua hata ya kuuza vitu vyao au kuingia kwenye mikopo yenye riba kubwa kwenye taasisiz a fedha ilimradi tu wapate fedha za kutulipia ada sasa ni wajibu wenu kukumbuka kwamba mna deni la kulipa na kulipa ni kusoma kwa bidii kuwarafiji wazazi ni kusoma kufika ngazi za juu,” amesema

Mkuu wa shule ya sekondari St Mary’s, Reca Ntipoo aliwapongeza wazazi na walezi wanaotambua ubora wa elimu inayotolewa na shule hizo na kuwapeleka watoto wao.

“Wamechagua jambo jema kwani pamoja na taaluma bora hapa kwani malezi na matunzo ya watoto ni mazuri sana kwani wanalelewa kwenye hali ya kuwa na hofu ya mungu na kutenda yaliyo mema,” amesema

Wahitimu wa kike wa kidato cha nne wa shule ya St Mary’s Mbezi jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye mahafali hayo ya 20 mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Shule Kuu ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUCE), Eugenia Kafanabo.

Amesema historia ya shule hiyo imekuwa ikipanda siku hadi siku na ushahidi wa hayo yote ni matokeo mazuri ya mitihani mbalimbali ya ndani na nje na wanafunzi wote wamekuwa wakichaguliwa kujiunga na vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi kutokana na ufaulu wao.

Amesema uvumilifu, juhudi, maarifa na kujituma ni nguzo muhimu katika mafanikio katika elimu na kwamba mahafali hayo ni uthibitisho wa uvumilivu wa wahtimu hao na kuwaasa kwamba mafanikio waliyopata yawe ngazi kwenye mafanikio katika ngazi zingine.