Na Mwandishiwetu,Timesmajira
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, imewataka wadau wa maendeleo yakiwemo mashirika na taasisi binafsi kuendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha hakuna mwanafunzi wakike anayekosa masomo kutokana kukosa Taulo za kike.
Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa Ripoti ya matokeo ya Uwekezaji katika kuondoa kodi kwenye Taulo za kike iliyopewa jina la umaskini na hedhi ambayo imefanywa chini ya Shirika la Msichana Initiative.
Afisa Elimu Mwandamizi kutoka Wizaraya Elimu,Sayansi na Teknolojia, Gladnes Kirei amesema ni kweli kuwa bado kuna baadhi ya mabinti wanaokosa elimu kutokana na changamoto ya umasikini hivyo kukosa kununua taulo za kike.
Amesema bado Serikali imeendelea kuchukua hatua kwa kushirikiana na wadau ili kuwasaidia wanafunzi wa kike kupata masomo bila changamoto.
“Wizara inafanya ongezeko la thamani la pedi kuhakikisha kila msichana anapata kwa bei nafuu .

“Pamoja na serikalikufanyahivyo kuondolewa ongezeko la thamani,utafiti huu utaleta chachu katika kuhakikishazinapatikana bila shida”,amesema
Kwa upande wake Mwakilishi wa UNICEF Tanzania,Eklke Wisch amesema kuwa suala la hedhi si la wasichana pekee bali ni suala la afya, elimu, usawa wa kijinsia na maendeleo ya taifa.
Amesema kwa muda mrefu hedhi imeendelea kuzungukwa na ukimya, unyanyapaa na taarifa zisizo sahihi hali inayowaathiri mamilioni ya wasichana na wanawake nchini Tanzania.
“Ripoti hii inaleta ushahidi muhimu utakaoisaidia Serikali na wadau kufanya maamuzi sahihi kuhusu namna ya kuboresha upatikanaji wa bidhaa za hedhi na kuondoa vikwazo vinavyowakabili wasichana na wanawake,” amesema.

Amesema UNICEF imeipongeza juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuendeleza agenda ya afya na usafi wa hedhi ikiwemo maandalizi ya Mwongozo wa Taifa wa Afya na Usafi wa Hedhi.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Msichana Initiative,Consolata Chikoti amesema kupitia ripoti hiyo imeonesha kuwa mahitaji ya taulo za kile nchini ni bilioni 3.3.
Amesema ili kukidhi mahitaji kwa wanawake zaidi ya milioni 18 zinahitajika ambapo ripoti hiyo inaonesha kufanya taulo za kike kama bidhaa muhimu ili kutoa unafuu katika upatikanaji wake
“Ripoti hii inatoa mwaliko kwa washirika wa maendeleo kuendelea kuwekeza katika suluhisho endelevu katika kuondoka kwenye majibu ya upande mmoja na badala yake kuchukua mtazamo wa kina unaojumuisha bidhaa nafuu za hedhi, uzalishaji wa ndani, maji safi, huduma bora za usafi wa mazingira, elimu kuhusu hedhi pamoja na kupunguza unyanyapaa.

“Tumekuwa tukizungumza kuhusu umuhimu wa maji safi na usafi wa mazingira, na tunaamini kuwa kila mdau aliyepo hapa ana nafasi muhimu katika kufanikisha agenda hii,”amesema

More Stories
Mradi wa pamba unavyosaidia kupiga vita Ajira za Watoto
Mshtakiwa wa tatu aunganishwa kesi ya mauaji
Mbeya City Expo yaelimisha wananchi bidhaa bandia