October 20, 2021

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yapongwezwa kwa ujenzi wa Daraja jipya Wami

Na Mwandishi wetu Timesmajira online, Pwani

BODI ya Mfuko wa Barabara (RFB)imeipongeza serikali kwa Kutekeleza mradi wa Ujenzi wa daraja jipya la Wami na Barabara unganishi ambao hadi sasa umefikia asilimia 55.6 na kutarajiwa kukamilika Septemba 2022.

Mradi huo wa ujenzi wa daraja jipya la Wami na Barabara unganishi unatekelezwa kwa fedha za serikali kuu kwa asilimia 100 na kutegenezwa na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Power Construction Corporation limited, kutoka nchini China kwa gharama ya Shilingi Billioni 67.779.

Akisoma taarifa fupi mbele ya watendaji wa Bodi ya Mfuko wa Barabara( RFB), baada ya kufanya ziara ya ukaguzi katika mradi huo Mkoani Pwani, Mhandisi Gabriel Sangusangu ambaye ni mshauri wa mradi huo amesema daraja hilo jipya lina urefu wa mita 510 na upana wa mita 11.85 linajengwa umbali wa mida 670 pembeni ya daraja la awali.

Amesema ujenzi wa daraja hilo, umekuja baada ya daraja la awali kutokidhi mahitaji ya magari yanayopita kutokana na kujengwa miaka mingi iliyopita na kueleza kuwa ni jembambana lenye njia moja.

“Daraja la awali lilikuwa na Barabara zinazounganisha daraja hilo ambazo ziko katika miinuko mikali na kona mbaya jambo ambalo limekuwa likisababisha ajali mbaya na vifo kutokea mara kwa mara katika eneo hilo”amesema Mhandisi Sangusangu.

Amesema, upana wa Ujenzi wa daraja jipya la Wami umezingatia sehemu ya barabara, watembea kwa miguu pamoja na vizuizi kwa ajili usalama pamoja na kujumuisha ujenzi wa Barabara za maingilio ya daraja kwa pande zote mbili zenye jumla ya urefu wa kilomita 3.8.

Mhandisi Sangudangu amesema, hadi kufikia sasa mkandarasi amekwishaleta asilimia 95 ya mitambo na vifaa vyote vinavyohitajika kwa ajili ya kazi ya Ujenzi .

Akifanunua zaidi kuhusu ujenzi wa daraja hilo Mhandisi Sangusangu amesema, kazi ya ujenzi wa misingi ya nguzo za daraja umekamilika kwa asilimia 100 huku ujenzi wa kuta mbili za mwanzo na mwisho wa Daraja ukiwa umekamilija kwa asilimia 85.

“Ujenzi wa nguzo namba 1 na 4 zenye urefu wa mita 19.6 umekamilika kwa asilimia 100 na Ujenzi wa nguzo namba 3 umefikia mita 44.1 sawa na asilimia 100 ya urefu mzima wa nguzi hiyi ambayi ndio ndefu zaidi kuliko zote”amesema Mhandisi Sangusangu

Aidha amesema awali ujenzi huo ulikuwa ukamilike Septemba 16 mwaka huu lakini kutokana na chagamoto mbalimbali ikiwemo kuchelewa kwa malipo ya mwaka jana kufika kipindi ambacho muda wa kumaliza mradi unakaribia kuisha.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB) Joseph Haule amesema, ujenzi wa daraja hilo ni wa kisasa tofauti na ujenzi wa daraja la awali ambalo ulilijengwa na mkoroni miaka 50 iliyopita.

“Kama mnavyoona daraja hili sio la mchezo daraja hili lenye njia mbili litakuwa la kisasa na kama tunavyojua gharama zote zinatoka serikali kuu tunaipongeza sana kwani Teknolojia zinazotumika katika ujenzi huu ni za hali ya juu “amesema Haule

Na kuongeza kuwa” uamuzi uliofanywa na serikali wa kujenga daraja hilo jipya kwa kutumia fedha za ndani ni mzuri na tunaona ujenzi unasimamiwa na Kampuni za ndani hivyo ufike wakati watanzania wanapaswa kutambua kuwa wanauwezo wa kutengenezwa vitu vikubwa zaidi ya hivi”aliongeza Haule

Naye Meneja Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) Mhandisi Andrea Kasamwa ameishukuru Bodi ya RFB kwa kutembelea mradi huo na kuhaidi kutelekeza maelekezo yote yaliyotolewa na Bodi hiyo kwa kuyafanyia kazi kwa uharaka

Amesema Tanroad itaendelea kusimamia ujezi huo wa mradi wa daraja la Wami ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na wananchi waweze kifaidika na daraja hilo.

Aidha amesema, jumla ya Shilingi millioni 700 zimetegwa kwa ajili ya maboresho na matengenezo ya barabara ya Bagamoyo hadi msata.