
Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Tarime
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na mafunzi wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Taifa, Kenani Kihongosi, amepongeza maendeleo ya Mradi wa Shule ya Sekondari ya Nyasaricho uliotekelezwa kwa thamani zaidi ya Sh. Bil 1.
Amesema, shule hiyo ya Sekondari ya wavulana na wasichana iliyojengwa kwa mtindo wa kisasa, itasaidie kuendelea kuboresha elimu kwa wananchi wa Tarime vijijini, huku akiwasisitizia kuendelea kuilinda miradi yote ya maendekeo iliyopelekwa kwa manufaa ya wananchi.

Kihongosi, ameipongeza Serikali chini ya Rais wake Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwajali wananchi wa Tarime vijijini na wananchi wote kwa ujumla kwa kuwapelekea kiasi cha Sh. Bil.1 ili kufanikisha mradi huo wa shule, huku Sh. Mil 6 zikiwa zimetolewa kutoka mapato ya ndani ya wilaya hiyo.
Aidha, amewataka wanafunzi wa shule hiyo, kusoma kwa bidii na kuwataka kuwa wazalendo kwa nchi yao na kutokubali kutumika kuharibu amani wao wakiwa kama vijana ambao ndiyo nguvu kazi nchini.
Shule ya Nyasaricho imejengwa kwa mtindo wa kisasa, yenye madirisha ya vioo na vigae ina vyumba vya madarasa 13, ofisi za walimu tatu huku mmoja akiwa mwalimu wa kujitolea, maabara za kisasa na chumba cha kulia chakula ‘Dinning’

Awali, Kihongosi alitembelea Shina namba moja, Tawi la Nyasaricho lililopo Tarime Vijijini, ambapo alizungumza na mabalozi na wanachama wa CCM, akiendelea kusisitiza kulinda uhai wa chama na kulinda amani.
Pia, amewataka viongozi wote wa chama hicho kuyavunja makundi, huku akisema kuwa huu ni wakati wa kukiimarisha chama na kusimamia ilani ya 2026/2030 ili kuhakikisha maendeleo ya wananchi yanapelekwa kama ilivyo pangwa.
“Kama kuna makundi hapa naomba miyavunje kwani CCM kinataka umoja na mshikamano na siyo makundi. Lakini pia niwataka viongozi hapa msibebe mtu badala ya chama, kwani kufanya hivyo ni kukigawa chama, CCM ni chama cha muda mrefu na kina taratibu zake hivyo takaye kiuka utaratibu chama hakitasita kumchukulia hatua.

Lakini pia, naomba niendelee kusisitiza juu ya kulinda amani ya nchi yetu, hapa Tarime pakiharibiwa hakutakuwa na sehemu nyingine ya kukimbilia, hivyo niendelee kuwasisitiza kulinda amani, kuna watu wamechanganyikiwa huko wanahamasisha watu kufanya vurugu, niwaombe msiwasikilize kwani akili za kuambiwa changanya na zako”, alisema Kihongosi.
Amesema, CCM ndiiyo chama pekee kinachotekeleza ilani yake kwa kuwaletea maendeleo wananchi kote nchini.



More Stories
Tabora yawapa motisha walimu
Kapinga: Serikali yaboresha Elimu, Afya, Kilimo Mbinga
Mwaselela: Rais Samia aimarisha ukaribu na wananchi