April 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali kuboresha minara 488 ktoka kasi ya 2G kwenda 4G

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

BENKI ya Dunia imeridhishwa na maandalizi ya utekelezaji wa Mradi wa Kidijitali ambao utagharimu kiashi Cha Shilingi bilioni 349 zilizotolewa na Benki hiyo wenye lengo la kuboresha minara 488 toka uwezo wa 2G kwenda 4G na zaidi ya minara mipya 300 itajengwa ili kuboresha huduma ya mawasiliano Nchini.

Akizungumza mbele ya ugeni huo,Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Injinia Mathew Kundo amesema kuwa  Mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miaka mitano   na utasaidia uboreshaji wa miundombinu ya TEHAMA ya Serikali,Miundombinu ya Taifa ya anwani za Makazi na posti Kodi,maendeleo ya Vijana na biashara ya mtandao.

Injinia Kundo amebainisha kuwa Mradi huo una lenga kukuza maendeleo ya Kidijitali kama kichocheo Kikuu Cha ukuaji wa uchumi na ukuaji wa Viwanda,utengenezaji wa ajira,utoaji wa huduma na ufanisi wa Serikali.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Dkt. Zainabu Chaula amesema kuwa atahakikisha ansimamia Mradi huo kwa weledi mkubwa na kuzingatia uwazi kama Benki ya Duniania inavyotaka kwakuandaa mfumo wa utoaji maoni huku  Mratibu wa Mradi huo,Honest Njau ameeleza namna Mradi huo utakavyotekelezwa pamoja na manufaa yake.

Kwa upande wake Justina Kajange ambaye ni  Mchambuzi wa mifumo  toka Benki ya Dunia akiongea kwa  kwaniaba ya kiongozi wa msafara Tim Kelly amesema Mradi huo ulikuwa na malengo ya muda mrefu toka Mwaka 2018 lakini wameridhishwa na maandalizi yake  hivyo Mradi utatekelezwa kama ulivyokusudiwa.