April 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Selikali yatenga bil. 149/-kufanikisha Bima ya Afya kwa Wote

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Dodoma

KWA kutambua umuhimu wa huduma za Afya kwa wananchi, Serikali imetenga kiasi cha Sh. bilioni 149 kwa ajili ya kuanza kutekeleza mpango wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote utakaoanza rasmi mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msingwa wakati akifungua mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Amesema, baada ya mjadala wa miaka mingi na juhudi mbalimbali za kuhakikisha wanajamii wanajiunga na huduma za Bima ya Afya zitakazowasaidia kupata matibabu kwa wote, hatimaye utelekezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote.

Amesema kuwa, Serikali ya awamu ya Sita kupitia kwa Rais Samia Suluhu Hassan imetenga bilioni 149 kwa ajili ya kufanikisha mpango huo ambao utaanza kwa makundi maalum ya wale ambao hawana uwezo wa kumudu gharaza za matibabu.

“Tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutenge bilioni 149 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote ambao utaanza rasmi mwaka huu kwa makundi yaliyokuwa na uwemo wa kumudu gharama za matibabu,” amesema Msigwa.

Pia ameweka wazi kuwa, kwa sasa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha mpango huo unatekelezwa hatua kwa hatua hadi Watanzania wote waweze kufikiwa na huduma hizo na tayari muswada huo utawasilishwa ndani ya Bunge litakalofanyika Septemba mwaka huu. 

“Japokuwa muswada huu utawasilishwa Bungeni mwezi ujao lakini kwa kutambua umuhimu wa jambo hili Serikali imetenga kabisa fedha ili muswada itakapopitishwa na sheria kuanza basi ukute kina kitu fulani kwa ajili ya kufanikisha mpango huu,”.

“Pia katika bajeti ya mwaka huu serikali imetenga trilioni 1.04 ambazo zitakwenda kuhudumia katika Halmashauri katika masuala ya Afya kwa kujenga vituo vya Afya, Zahanati, Hospitali, kununua dawa na pamoja na mambo muhimu, lakini pia wamechukua hatua nyingine nyingi ikiwemo fedha za mapato kutoka kwenye Mikoa ambazo ni karibu bilioni 13 kuanzia mwezi huu ambazo zimeelekezwa kuwa asilimia 50 ikanunue dawa kwa ajili ya Watanzania,” amesema Msigwa.

Akimkaribisha mgeni rasmi katika mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bernard Konga, amesema katika kuadhimisha miaka 20 ya kuanzishwa kwa  NHIF , umeandaa mkutano na wahariri wa vyombo vya habari nchini Ili kujadili masuala yanayohusu huduma zake kwa kuangalia walikotoka, waliko na wanakoelekea.

Amesema kuwa kuna mafanikio mbalimbali yamepatikana tangu kuanzishwa kwa mfuko huo