May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Picha ya juu ikionesha mitaa ya mji Mtakatifu wa Mecca mapema mwezi huu ikiwa hauna watu kutoka na mapambano ya virusi vya COVID-19. Picha na AP

Sala za Taraweeh wakati wa Ramadan kusitishwa

Na Mwandishi Wetu

DUBAI, Wizara ya Mambo ya Masuala ya Waislamu na Miongozo katika Umoja wa Falme za Kiarabu imetangaza kusitishwa kwa sala za Taraweeh wakati wa mfungo wa Ramadan na badala yake zitafanyika nyumbani.

Hatua inayochukuliwa ikiwa pia sala katika misikiti imezuiwa hadi pale ambapo virusi vya corona (COVID-19) vitadhibitiwa.

Gazeti la Al Riyadh limemnukuu Waziri wa wizara hiyo, Dkt. Abdul Latif Al Sheikh akisema, “kusimamishwa kwa sala tano za kila siku katika misikiti ni muhimu zaidi kuliko kusimamishwa kwa sala za Taraweeh. Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu akubali maombi ya Taraweeh iwe imefanyika katika misikiti au nyumbani, jambo ambalo tunadhani ni bora kwa afya ya watu.

“Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu akubali maombi kutoka kwetu sisi sote na kulinda ubinadamu wetu kutokana na janga hili ambalo linasumbua ulimwenguni kote,”amefafanua Dkt.Al Sheikh.

Kwa kina jisomee katika gazeti la Majira…