May 14, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rehmtula awakaribisha wadau wa mitindo kwenye mnada

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MBUNIFU mkongwe wa mavazi, Ally Rehmtula ana

wakaribisha wadau wa mitindo na wateja wake katika

mnada wa mavazi ya kitenge na liner, ambao

utakutanisha watu mbalimbali wa tasnia ya mitindo

ofisini kwake Masaki Chole, jijini Dar es Salaam.

Rehmtula ni miongoni mwa wabunifu mahiri hapa nchin

ambao wanapenda kutengeneza nguo zao kwa kutumia

maligafi za kiafriaka.

Akizungumzia hilo Rehmtula amesema, siku hiyo kutakuwa

na nguo za jinsi ya kike na kiume na rika zote, mavazi

hayo yatakuwa na punguzo maalum.

“Nimeandaa mnada huu ili kukutana na wadau wa tasnia

pamoja na wateja wangu, hivyo kila bidhaa itakuwa na

punguzo la asilimia 20 hii ni kwa sababu ya kurudisha

shukurani kwa jamii inayo nizunguka,” amesema

Rehmtula.

Amesema, mnada huo utafanyika Julay 3 kuanzia asubuhi

mpaka jioni, kutakuwa na viongozi wa serikali na

mastaa kutoka tasnia tofauti ambao wamekuwa wakifanya

kazi na mbunifu huyo.