April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rashford: Sitoomba msamaha kamwe

LONDON, England

MSHAMBULIAJI wa Manchester United na timu ya Taifa ya Uingereza, Marcus Rashford amesema hataomba msamaha kamwe

kwa ni yeye ni nani?, baada ya kupokea unyanyasaji wa kibaguzi, kufuatia Uingereza kushindwa kutamba kwenye mchezo wa fainali ya Euro 2020 dhidi ya Italia na kukubali kichapo kwa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya dakika 120 kutoka sare ya gili 1-1.

Rashford, mwenye umri wa miaka 23 raia wa Uingereza alikuwa mmoja wa wachezaji watatu,

pamoja na Jadon Sancho na Bukayo Saka, ambao walikosa penalti na kuanza kuchambuliwa kwa ubaguzi wa rangi.

Hata hivyo, Rashford amekuwa shujaa kwa wengi nje ya serikali nchini humo kutoa chakula bure mashuleni kwa watoto wasio na uwezo baada ya kukumbwa na janga kubwa virusi vya korona.

“Mimi ni Marcus Rashford, mtu mweusi wa miaka 23 kutoka

Naington na Wythenshawe, Kusini mwa Manchester. Ikiwa nina

au sina kitu kingine chochote kile, “Rashford ameandika katika taarifa

kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Rashford, ambaye aliingia kipindi cha pili katika mchezo wa fainali ya Euro 20202 aliomba msamaha kwa kukosa kwake penalti.

“Ninaweza kukosoa utendaji wangu siku nzima, jamani

adhabu haikutosha, inapaswa kuingia lakini

Kamwe sitaomba msamaha kwa mimi ni nani na wapi nilikuja

kutoka,”Rashford ameongeza.