Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi watatu wakiwemo wajumbe sita wa bodi.
Taarifa iliyotolewa leo Mei 3, 2021 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Athman Kattanga imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hao umetenguliwa kuanzia Aprili 30, 2021.
Kwanza, Mhe. Rais Samia ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Prof. Tadeo Andrew Satta.
Sambamba na hatua hiyo, Rais Samia pia ametengua uteuzi wa wajumbe sita wa bodi ya TASAC. Pili, Rais Samia ametengua uteuzi wa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Hassan Mwang’ombe.
Tatu,Rais Samia ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania Dkt. Harun Kondo.Sambamba na hatua hiyo, Mhe. Rais Samia pia amevunja Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania.
Uteuzi wa viongozi watakaoshika nyadhifa hizo utafanywa baadaye.

More Stories
T-CAMS yaleta mapinduzi sekta ya uwakala wa forodha
Mafuta ya zabibu yavutia Nanenane
Nanauka apongeza Kariakoo Kwa kuwezesha vijana Kibiashara