May 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia apongeza ushindi wa Yanga

Na Mwandishi Wetu,Timesmajira Online, Dar

RAIS Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Yanga kwa ushindi wa magoli manne dhidi ya CR Belouzdad ya Algeria na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Rais Samia ametoa pongezi hizo jana kupitia kupitia mtandao wake wa Instagram.

“Naipongeza Klabu ya Yanga kwa kufanya vyema katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), na kufanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali.

Mafanikio haya yameandika historia kubwa kwa klabu na sekta ya michezo nchini. Mmeleta furaha kwa mamilioni ya mashabiki wenu na Watanzania kwa ujumla,” ameandika Rais kupitia Instagram.

Mechi ya jana ikwenye Uwanja wa Mkapa, ambayo ilipewa jina la ‘Pacome Day’ jina la mchezaji,Pacome Zouzoua ilinogeshwa na mtindo wa rangi kwenye nywele kuanzia mashabiki, wachezaji hadi viongozi wa timu hiyo.

Baada ya mechi hiyo kumalizika Yanga ilipokea sh. milioni 20 kutoka kwa Rais Samia kupitia kampeni ya Goli la Mama yenye lengo ya kuhamasisha timu kufanya vizuri katika michezo ya kimataifa.