Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania itatenga eneo la ekari 20 katika mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuhudumia mizigo kutoka Zambia.
Rais alitoa kauli hiyo wakati akitoa hotuba kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi.
Zambia ni mteja mkubwa wa bandari ya Dar es Salaam, ikichukua asilimia 34 ya mizigo yote inayopitia bandari hiyo kwenda nje ya Tanzania.
Rais Samia alitumia fursa hiyo kusema kwamba mipaka ya kijiografia baina ya Tanzania na Zambia haipaswi kuwa kikwazo cha biashara na uwekezaji baina ya nchi jirani.



More Stories
Chatanda ahamasisha utekelezaji wa Ilani ya CCM 2025–2030
Mikopo asilimia 10 yainua wanawake Tunduma kibiashara
UDSM yabuni bidhaa kwa nazao ya nyuki