May 14, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

P-Funk ajikita uandaaji wa filamu

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MKURUGENZI wa Studio za Bongo Record Paul Matthysse

maarufu kama ‘P Funk’, ameamua kuachana na kazi ya

kuandaa muziki na hatimaye kujikita kwenye uwandaaji

wa filamu kwa ajili ya kutafuta changamoto nyingine.

Akiweka wazi hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa

Instagram P Funk amesema, ameishi maisha ya studio kwa

muda wa miaka 28 kwa ajili ya kusikiliza vyombo vya

muziki usiku na mchana hivyo hana budi kufanya mambo

mengine.

“Nimeishi Studio Life kwa zaidi ya miaka 28, Miaka 28

ya kusikiliza kelele za vyombo vya Muziki usiku na

mchana, Miaka 28 ya Kuandaa Nyimbo za Watu tofauti,

Waliofanya vizuri katika nyakati tofauti.

“Maisha na Umri Vimeniintroduce kwenye Ulimwengu

mwingine, ni muda ambao nahitaji zaidi utulivu, Ku-

enjoy Nature, Kusafiri Sehemu tofauti nikiwa na

Camera, tuwe pamoja katika Career yangu mpya ya Film

Making Aand Video Production. Asanteni na karibuni

katika safari yangu,” amesema P Funk.