April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ndugai azitaka Asasi za Kiaia kujitathimini,kufanya kazi kwa weledi

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma


ASASI za kiraia nchiniĀ  zimetakiwa kutoruhusu migongano,migogoro na kuzingatia kufanyakazi kwa weledi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.


Hayo yameelezwa leo jijini hapa na Spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai katika maadhimisho ya wiki ya asasi za kiraia ( Azaki)Ā  yanayofanyika Jijini Dodoma ambapo amesema ni wakati wa asasi hizo kujitathimini na kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria zinazowaongoza.


“Hata kama Asasi za kiraia zinatoa mchangoĀ  mkubwa katika kujenga nchi lakini endapo mtaruhusu migogoro na migongano ndani ya asasi zenuĀ  itakuwa ni jambo gumu kwenu kufanikisha malengo au hazma walizo mlizojiwekea.


Naye muwakilishi wa asasi ya wote sawa inayojishughulisha na Utoaji Elimu na kutetea wafanyakazi wa majumbani Jenipher Kato, amesema kuwa katika wiki ya asasi za kiraia wanatumia kuelimisha jamii kuhusu wafanyakazi wa majumbani ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya umuhimu wa kuwapa wafanyakazi wa ndani mikataba.


Wiki ya asasi za kiraia inafanyika Jijini Dodoma ambapo asasi mbalimbali zinapata nafasi ya kukutana na kujadili mambo yanayohusu asasi hizo pamoja na kutoa Elimu mbalimbali kwa jamii.