April 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nderiananga atoa maagizo kwa wenye ulemavu nchini

Na Hadija Bagasha,timesmajira,online

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu –Watu wenye Ulemavu Ummy Nderiananga amelitaka Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania (Shivyawata) kuacha fitina, figisu na  migogoro kwani haina  tija na itapelekea kuwachelewesha kufikia malengo yao.

Naibu waziri Nderiananga ameyasema hayo leo wakati wa Kongamano la kuelekea siku ya wenye ulemavu duniani ambapo kitaifa litafanyika kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga ambapo amesema kuna watu mabingwa wa kutengeneza makundi kwenye vyama vya wenye ulemavu na kusababisha kushindwa kutekeleza wajibu wao

 Naibu waziri Ummy amesema ni lazima wabadilike na kuondokana na dhana ya kuipa nafasi migogoro badala yake wasaidiane ili waweze kutimiza malengo yao kutokana na kwamba hakuna kitu kinachochelewesha kufikia malengo yaoe kama hicho ikiwemo kushirikiana kwa pamoja na kupendana wao wenyewe

“Ndugu zangu pendaneni, saidianeniuongozi ni kuchukuliana kusaidiana acheni chokochoko ukinichokonoa mimi nikadondoka utadondosha na wengine hivyo niwasihi achaneni na mambo hayo badala yake shikaneni”Amesema

Akizungumza mkakati wa serikali kuendelea kuboresha huduma kwa kundi la watu wenye ulemavu ambapo amesema Rais Samia Suluhu  Hassan amewapa fedha kiasi cha Bilioni 8 kwa ajili ya kujenga vyuo vipya vya ufundi kwa watu wenye ulemavu.

Amesema ujenzi wa vyuo viwili utakwenda sambamba na kukarabati vilivyopo na kwa kuanzia ikiwemo kujenga chuo nyanda za juu kusini ikiwemo Mkoa wa Songwe Halmashauri ya Mbozi.

Aidha amesema chuo kingine kitajengwa wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma ambavyo ni vyuo vipya na michoro yake imekwisha ambao walikuwa wanashirikiana na wahandisi na wamemaliza.

“Niwaambie kwamba Rais Samia ameweka pesa tayari ipo hazina wanasubiri michoro ipelekwe na tumepiga hatua na Rais analidhamini sana kundi letu na vyuo vyetu vilivyobakia vyote vikae kwenye mfumo mmoja vipendekeze”Amesema

“Nataka niwaambie hapa Tanga kuna chuo cha Masiwani cha watu wenye ulemavu na Serikali inaboresha vyuo vyote na Rais Samia ametoa fedha milioni 4 kupitia Tamisemi kujenga mabweni ya wanafunzi wenye ulemavu kwenye shule za Msingi yatajengwa mabweni 50 na hapa Tanga tutajenga mabweni mawili yameeshaanza na yanaendelea vizuri”amesema

Hata hivyo amesema wameamua kufanya hivyo kutokana na kwamba wanafunzi wenye ulamavu wanatapa shida ya umbali na Rais Samia ameliona hilo na ametoa fedha hizo ili wanafunzi wakae shuleni wasome na kuondokana na changamoto ambazo walikuwa wanakabiliana nazo awali.

 “Tunampongeza Rais wetu Samia Suluhu na tuendee kumuunga mkono  kwani amedhamiria kuhakikisha changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu zinapatiwa ufumbuzi”Amesema

Hata hivyo Naibu Waziri Ofisi ya waziri huyo amesema serikali imetoa bilioni nane  kwa ajili ya vyuo vya ufundi kwa watu wenyeulemavu nchini.

Ni kongamano na kuelekea siku ya watu wenye ulemavu duniani  ambayo kitaifa  itafanyika jijini Tanga.

Kwenye kongamano hilo  naibu waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu ,watu wenye ulemavu Ummy Nderiananga anazungumzia bilioni 8 zaRais Samia  kwenye ujenzi wa vyuo vya ufundi.

Washiriki wa kongamano hili , akiwemo Tongi Mwanjala Makamu Mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu SHIVIAWATA  wamesema,  fedha hizo zitasaidia watu wenye ulemavu kujifunza  masuala mbalimbali na kujikwamua kiuchumi.

Siku ya watu wenye ulemavu duniani huadhimishwa  kila ifikapo desemba 3 wakati ambao watu wenye ulemavu wanakutana na kupata  nafasi ya kupaza sauti zao dhidi ya changamoto zinazowakabili.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimishi ya siku hiyo.