Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hapa nchini kwa upande wa wanawake Faustina Charles maarufu ‘Nandy’, amethibitisha kutolewa barua na aliyekuwa mpenzi wake Billnass.
Akithibitisha hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Nandy amesema, kwa sasa yeye ni mke mtarajiwa kwani tayari ameshatumiwa ujumbe kuwa barua ya mpenzi wake aliyepeleka kwao imepokelewa.
“Nimepokea ujumbe kuwa barua yake imepokelewa nyumbani. Hivyo kwa sasa mimi ni mke mtarajiwa (wife to be),” ameandika Nandy kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram.

More Stories
Burudani zapamba utambulisho wa ‘Fanta Berry’ nchini
Chief Hangaya Festival kufanyika Aprili 19,2026
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wakiburudika kusubiri Uzinduzi Ilani ya CCM 2025-2030