March 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nandy aifagilia mgoma yake ‘Nimekuzoea’

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa kike anayefanya vizuri katika kiwanda cha Bongo fleva Faustine Charles maarufu ‘Nandy’, ameusifia wimbo wake ‘Nimekuzoea’ baada ya kufanya vyema katika mtandao wa Shazzam wiki hii.

Akitoa sifa hizo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Nandy amesema, amefarijika sana baada ya kuona wimbo huo umeshika nambari moja Afrika Mashariki.

“Nimekutana na playlist ya ngoma zilizotafutwa zaidi kwenye mtandao wa Shazzam kwa wiki hii Afrika mashariki, kwa mujibu wa Apple music, na Nimekuzoea imeshika namba 1 hapo!,” amesema Nandy.