Na Yusuph Mussa, Timesmajiraonline,Dodoma
WAZIRI wa Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, ametaka kufanyike juhudi za pamoja kati ya wizara, taasisi za Serikali na wadau wa maendeleo kuona wanashirikiana ili kuwasaidia vijana kiuchumi.
Akizungumza Agosti 7, 2026 kwenye Banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) lililopo katika Maonesho ya Kilimo (Nanenane) Viwanja vya Dkt. John Malecela, Nanauka alisema kuna fursa nyingi zinatolewa kwa vijana, hivyo lazima waziratibu kwa pamoja.

“Na sisi kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, mambo mengi yapo kwenye value chain (mnyororo wa thamani) ya kilimo na ufugaji, na hata wiki mbili zilizopita tulikuwa Ludewa, tulipeleka kizimba kwenye Ziwa Nyasa. Najua ninyi hamjaanza, lakini wao kama halmashauri waliweka pesa, wafanye majaribio, na wakaona kama ina matokeo, na sisi tulikwenda kuongeza nguvu, na nimezungumza na Waziri wa Mifugo na Uvuvi tuone namna ya kuwaongezea nguvu.
“Kikubwa ambacho nataka kusisitiza ni coordination (uratiushirikiano), tuna changamoto kubwa sana kwenye taarifa. Sasa hivi tuna Wizara ya Vijana, hivyo kijana yeyote akisikia jambo linalohusu kijana, anakuja kwetu, na kusema amejaribu kuomba aidha mkopo na anaelezwa sijui kuna Mfuko wa Dhamana na kunahitajika dhamana, lakini akija kwetu sisi tunakuwa hatuna taarifa ya kujitoshleeza” amesema Nanauka.
Nanauka amesema kwa muktadhs huo, Taasisi za Serikali na wadau wrngine, wanapokaa na kupanga utekekezaji wa shughuli za vijana iwe ni mikopo ama shughuli nyingine za kiuchumi, basi washitikiane kwa pamoja ili taarifa sahihi ziwe zimefika kila mahali.

Nanauka amesema nia ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni njema ys kuhakikishs vijana wanainuka kichumi, hivyo kukiwa na uwajibikaji na utoaji taarifa kwa pamoja, wataweza kufikia matamanio ya Rais kuona vijana wanainuka kiuchumi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mipango, Ushauri na Mambo ya Taasisi wa Benki ya TADB, Mkani Waziri amesema wamepokea fedha sh. bilioni 18.7 kutoka serikalini kwa ajili ya kuwakopesha vijana bila riba, na zaidi ya vijana 1,900 wameshatuma maombi, na maombi hayo wanayachakata ili kuweza kuwakopesha fedha hizo.
Waziri amesema kwa upande wa Mfuko wa Dhamana, wanafanya kazi na benki 21, hivyo vijana wanapokuwa na miradi ya kibunifu, na wakaenda kwenye hizo benki na wakawa na chsngamoto ya dhamana, Benki ya TADB inawawekea dhamana hadi asilimia 70 ili waweze kupata mikopo kutoka kwenye hizo taasisi za fedha.

Lakini kwa upande wa mikopo ya ndani ya Benki ya TADB, kuna mikopo haina riba kabisa kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, na kuna mikopo yenye riba ya asilimia tano.
“Tuna mradi unafahamika kama Solidaridad tunaufanya Tanga kama mradi wa majaribio, lengo kubwa ni kuhakikisha vijana wanapata ajira kwenye Sekta ya Mifugo. Kule tulichokifanya vijana wanaokuwa kwenye mazingira yao ya vijijini tunawapa mtaji unaowasaidia kupata shamba la ekari 10, wanajengewa nyumba na banda la kutosha ng’ombe 10, wanaanzishiwa banda la kuku, na wanakuwa na shamba la malisho kwa ajili ya kulisha mifugo yao.
“Baada ya hapo tunawaunganisha na mnunuzi wa maziwa, na kwa kule Tanga tunafanya kazi na Tanga Fresh. Kwa upande wa uvuvi, tukishirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, tumeendelea vizuri hususani eneo la vizimba. Sasa hivi tumeshaweka vizimba 703 kwenye maziwa mawili, Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria. Ziwa Victoria tunafanya kwenye mikoa mitano vipatavyo 674, lakini Ziwa Tanganyika tumeweka vizimba 29 kwenye mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa” amesema Waziri.




More Stories
TAHA yabuni teknolojia mpya za bustani za nyumbani
Watakiwa kuacha uchimbaji holela wa Visima
Wakulima zaidi ya 200 wapatiwa elimu matumizi ya viuatilifu