April 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Naibu waziri wa maji Mhandisi Mahundi  aonya wanafunzi wa kike kutotumia vibaya sera ya elimu


Na Esther Macha,Timesmajira,Online,Mbeya

WANAFUNZI wa kike wametakiwa kutoitumia vibaya sera ya elimu na kwamba Serikali imewekeza wanafunzi wanaopata ujauzito Shule wakijifungua warejeshwe kuendelea na masomo hivyo sera hiyo isitumike kwao kufanya ngono zisizo salama.

Hayo yamesemwa leo na  Naibu waziri wa maji na Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Mbeya ,Mhandisi Maryprisca Mahundi wakati aliposhiriki uzinduzi wa wimbo wa kuelimisha wanafunzi na jamii kujikinga na magonjwa ya zinaa kupitia Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na kuhusishwa wanafunzi zaidi ya 60 wa Shule ya Sekondari ya Wasichana na Loleza Jijini hapa.

Mhandisi Mahundi amesema kuwa wanafunzi wanatakiwa kutoitumia vibaya elimu wanayoipata  kwani wazazi na Serikali wamewekeza kwao ili kuja kuishi maisha mazuri na kazi nzuri sasa kitendo cha kushindwa kusoma kwa budii na kudanganyika na bodaboda kinawapotezea muda .

”Taarifa ya Shule imenisikitisha sana kwa shule yenye vipaji kama hii  vya wanafunzi na kutoa wanafunzi bora kuwepo kwa baadhi yenu kuacha masomo  kutokana na kupata ujauzito jambo ambalo halipendezi”amesema Naibu waziri .

 Kwa upande wake mtafiti kutoka Taasisi ya  Magonjwa ya Binadamu (NIMR) mkoani Mbeya Dkt.Ruby  Mcharo amesema wastani wa asilimia 21 ya wanafunzi 504 wa  Vyuo Vikuu nchini waliopimwa wamebainika kuwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa  wanawake ni asilimia 21 huku wanaume  asilimia 14 kwa takwimu za mwaka 2019/2021.

Aidha Dkt.Ruby amesema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya makundi ya vijana wenye umri kati ya miaka 18 mpaka  21 kukutwa na magonjwa zinaa licha ya kuwepo kwa kampeni za utoaji elimu ya mara kwa mara  ili kunusuru kundi hilo inayotolewa na watafiti kutoka NIMR kwa kushirikiana na wataalam wa afya.

”Tafiti za maambukizi kwa wanavyuo ni kubwa na Changamoto kubwa ni kufanya ngono na zinaa zisizo salama na wameona sasa kuwafikishia elimu kwa njia za wimbo kwa makundi mbalimbali ”amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ,Dkt. Rashid Chua chua , amesema  Shule ya Sekondari ya Wasichana Loleza imekuwa ikifanya vizuri sana katika masuala ya afya hivyo ni wakati sasa kwa Taasisi hiyo  kuongeza weredi kwa kutoa elimu bora ya kujikinga na magonjwa ya zinaa.

Mwanafunzi wa kodato cha Sita ambao wako kwenye mradi huo ,Catherine Mwajebele ameomuomba Naibu Waziri kuendelea  kuwakumbuka na kuwashika mkono kupitia Taasisi yake ya Maryprisca Women Empowerment fund.