Na Mwandishi wetu,Timesmajira
MWANASHERIA Harrieth Ndege ameeleza namna alivyoguswa kwa kina na hotuba ya Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi, hasa katika masuala yanayohusu haki, ustawi na maendeleo ya wanawake nchini.
Kutokana na msukumo huo, Harrieth ameungana na Mwanaharakati mzawa Alphonce Muyinga katika juhudi za kujitolea kwa jamii, ambapo walifika katika Shule ya Msingi Michese, Dodoma, kutoa msaada na hamasa kwa wanafunzi.

Aidha, Harrieth amebainisha kuwa miongoni mwa viongozi wanaomvutia kwa utendaji kazi wao ni Dorothy Gwajima, akieleza kuvutiwa na jitihada zake katika kulinda na kutetea haki za mtoto wa kike.
Katika kuonesha kwa vitendo dhamira yake ya kusaidia jamii, Harrieth ametoa msaada wa taulo za kike (sanitary pads), toilet paper na sabuni, ili kusaidia watoto wa kike kujisitiri na kuzingatia usafi wa mwili, hatua inayochangia kuboresha afya na kujiamini kwa wanafunzi hao wakiwa shuleni.

More Stories
Serikali yaweka mazingira rafiki kuvutia uwekezaji sekta ya elimu
Mixx yakabidhi zawadi kwa washindi watatu Sabasaba
Serikali yaahidi kuendelea kuunga mkono Wawekezaji wa Usafiri wa Umeme