Na Zena Mohamed,TimesmajiraOline,Dodoma.
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi wa (CCM)Kenani Kihongosi,amesema chama hicho kimeipokea ripoti ya matukio ya ghasia yaliyotokea Oktoba 29, 2025 kwa uzito mkubwa kikitambua mchango wake katika kulinda mshikamano wa taifa na kujenga msingi imara kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Kenani amesema hayo jijini hapa leo Mei 4,2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema lengo Kuu la Tume hiyo ni kusaidia Taifa kujifunza kutokana na matukio yalitokea pamoja na kuimarisha umoja wa kitaifa jambo ambalo amesema CCM inalipa kipaumbele kikubwa.
Alieleza kuwa moja ya malengo makuu ya tume hiyo ilikuwa ni kusaidia taifa kujifunza kutokana na matukio yaliyotokea pamoja na kuimarisha umoja wa kitaifa, jambo ambalo CCM inalipa kipaumbele kikubwa.
“Chama cha Mapinduzi kinampongeza Mwenyekiti wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuunda tume hiyo kwa mujibu wa sheria za nchi, ikiwemo sura ya 32 ya sheria za Tanzania,”amesema.
Aidha Kenani amesema kuwa hatua hiyo inaonesha dhamira ya dhati ya uongozi katika kusimamia haki, uwazi na uwajibikaji.
Aidha, chama hicho kilisifu utendaji wa tume hiyo kwa kufanya kazi kwa uhuru, weledi na uzalendo wa hali ya juu. Pongezi maalum zilitolewa kwa Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Othman Chande, pamoja na wajumbe wote waliotekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa.
CCM pia iliwashukuru Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi kutoa maoni na ushahidi wao kwa utulivu na ushirikiano mkubwa wakati wa zoezi la ukusanyaji wa taarifa, jambo lililosaidia kukamilika kwa kazi ya tume hiyo kwa mafanikio.
Kuhusu mapendekezo yaliyotolewa, CCM imeeleza kuyaunga mkono kikamilifu na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuyapokea na kuonesha utayari wa kuyafanyia kazi kwa manufaa ya taifa.
Chama hicho kiliahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu katika utekelezaji wa mapendekezo hayo, pamoja na kuwahamasisha Watanzania kuunga mkono hatua zitakazochukuliwa ili kuimarisha umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa.
Hata hivyo, CCM ilisisitiza kuwa njia sahihi ya kufikia suluhu ya kudumu ni kupitia maridhiano ya kitaifa, sambamba na kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo halisi cha ghasia hizo, waliohusika, malengo yao na hatua stahiki za kuwawajibisha wahusika.

More Stories
Mwanasheria Ndege,Mwanaharakati Alphonce waunga mkono jitihada za Serikali
Waandishi 3,357 wapata Ithibati kupitia mfumo maalum
Samia atoa bil 20,waandaji maudhui wanufaika