October 20, 2021

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwamko wa wananchi kuchanja chanjo ya UVIKO-19 waongezeka Songea

Na Jacquelen Clavery,TimesMajira Online,Songea

WANANCHI wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wameendelea kuhamasika kuchanja chanjo ya UVIKO-19 baada ya kuelimishwa na kushuhudia madhara mbalimbali yatokanayo na ugonjwa wa UVIKO -19.

“Tumepata hamasa ya kuchanja kupitia elimu mbalimbali zinazotolewa na Wataalam wa Afya ,Viongozi wetu kupitia vyombo vya habari “,alisema mmoja wa wanakijiji cha Liweta Laurensia Komba.

Naye Emilani Mwingira ni mkazi wa kijiji cha Liweta kilichopo Kata ya Mpandangindo Halmashauri ya Wilaya ya  Songea amesema kwa sasa wananchi wamehamasika kuchanja kutoka na Elimu inayotolewa na Wataalam wa Afya,Viongozi mbalimbali wa Dini,Chama na Serikali na shuhuda za vifo vinavyokana na ugonjwa huo.

Wametoa wito kwa Serikali kuendelea kuwaletea chanjo ya UVIKO -19 kwasababu watu wengi bado hawajapata huduma  ya chanjo na wamehamasika kuchanja kwa hiari  baada ya kupata elimu na kutambua madhara ya ugonjwa ya kiwemo baadhi yao kuwapoteza wapendwa wao kwa vifo na baadhi ya familia kuyumba kiuchumi na kusambaratika.

Kwaupande wake moja ya Wataalam wa Afya Adam Ngunga waliofika kijijini hapo kwalengo la kutoa Elimu na zoezi la kuchanja amesema Serikali kupitia  mpango wahuduma   Shirikishi  na Harakishi ndani ya siku 14 uligawa dozi 2000 kwa Halmashauri hiyo kwa nia ya kuwachanja wananchi wake.

Ngunga amesema dozi hizo zimekuwa chache ukilinganisha na mahitaji halisi ya wananchi katika maeneo mbambali ya  ndani ya Halmashauri hiyo na kusababisha  baadhi ya wananchi kukosa chanjo,hivyo wawe sna subira wakati juhudi nyingine zikifanyika za kuwapelekea huduma hiyo

Naye Mganga Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Jairy Khanga amesema huduma ya Chanjo ya UVIKO-19 itamfikia kila mwananchi mwenye kuhiari kuchanja popotea alipo kwalengo la kupambana na ugonjwa huo huku akitoa msisitizo wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga.

Kwa Mkoa wa Ruvuma Halmasahauri ya Wilaya ya Songea imeongoza kwa zoezi la uchanji kupitia mpango maalum wa Serikali wa huduma ya Shirikishi na Harakishi kwa kuchanja zaidi ya asilimia 100 baada ya wananchi kuwa na mwamko mkubwa wa kuchanja na chanjo kutokidhi mahitaji ,hivyokulazimika kuomba chanjo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Mkoa.

Halmashauri ya Wilaya ya Songea inajumla ya vituo 37 vya kutolea huduma  za Afya kati ya hivyo vituo vitano havitoi huduma za chanjo kutokana na ukosefu wa miundo mbinu ya kuhifadhia vifaa hivyo  ambavyo ni Matimira,Magagura,Lipaya,Mbingamhalule na Lugagara.