May 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwalongo: Viongozi badilisheni mtazamo kwa wakulima

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

VIONGOZI wapya wa chama cha wakulima kanda ya nyanda juu kusini (TASO)wametakiwa kubadilisha mitazamo kwa wakulima kuona kwamba kilimo ni kama kazi nyingine ambayo inaweza kubadili maisha ya mkulima na kuwa na maisha bora na kuachana na dhana kudharau kilimo.

Mwenyekiti wa chama cha wakulima Taifa (TASO), Isdory Mwalongo amesema hay leo wakati wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa viongozi Taso kanda ya mbeya uliofanyika jana mkoani Mbeya katika ukumbi wa mikutano uliopo eneo la Nane nane.

Amesema kuwa viongozi wapya waliochaguliwa wakawe mstari wa mbele kusaidia wakulima kutokana na changamoto walizonazo hivyio kama vuiongozi bado wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa wanabadilisha mtazamo kwa wakulima na kuona kilimo ni kama kazi zingine wanazofanya watu ambazo zinaweza kuwaletea kipato.

“Ndugu zangu mnaogombea mnafahamu changamoto za wakulima hata juzi hapa kumetokea mgongano na serikali hili halituhusu ,kazi yetu sisi viongozi ni kuhakikisha tunabadilisha mtazamo kwa wakulima wetu ili waweze kusonga mbele”amesema Mwenyekiti huyo .

Aidha Mwalongo amesema chama hicho cha wakulima hakipingani na serikali wanafanya kazi kwa misingi ya kutelekeza ilani ya chama cha mapinduzi ya kiongozi aliyeyopo madarakani kwa maana hiyo wanafanya kazi kwa mtazamo wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wao hawapo hapo kama cha siasa.

“Siisi hapa tupo katika kuhakikisha kuwa wakulima wetu wanakuwa na amani na kufanya kazi vizuri na kubadilisha maisha yao na kuhakikisha kuwa wanakuwa katika hali nzuri ya kimaisha “amesema.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa chama cha wakulima Tanzania (TASO )Ramadhani Kiboko amesema kuwa chama hicho kilizinduliwa rasmi Februari 27 mwaka 1993 kikiwa na wanachama waanzilishi 17 na kuwa mpaka sasa wana wanachama 1,133.

Aidha Kiboko amesema kuwa lengo kubwa ni kuhakikisha shughuli za kiklimo, ufugaji na ushirika nchini kwa kutumisa mbinu mbakli mbali ikiwemo kuandaa na kuratibu maonesho ya kilimo yanayoaambana na na maadhimisho ya sikukuu ya wakulima Nane nane ambayo hufanyika kila mwaka.

Mkutano mkuu huo umemchagua Ramadhani Kiboko kwa kupata kura 24, kuwa Mwenyekiti wa chama cha wakulimaTanzania kanda ya nyanda za juu kusini (TASO) nafasi ya Katibu mtendaji wa Taso Kanda ilikuwa na mgombea mmoja ambaye ni Daudi Mwalusamba aliyepata kura 25 ,kwa upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nafasio hiyo ilikuwa na wagombea watatu ambao ni Aron Mwalughelo kura 12 ,na Khadija Mohamed alipata kura 11 na Joel Samweli aliyeambulia kura tatu na mtunza hazina ni Habakuki Nsyenge viongozi wote waliochaguliwa katika nafasi hizo watadumu kwa muda wa miaka mitano.

Akizungumza katika mkutano huo aliyekuwa Mwenyekiti wa Taso kanda ya Mbeya ,Crispin Mtono amesema kuwa ameamua kuachia nafasi hiyo wanachama wengine waongoze hasa vijana ili chama kiweze kusonga mbele .