May 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mtoto alipukiwa na bomu, afariki

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Kigoma

MTOTO wa miaka 9 katika Kijiji cha Kasumo Kata ya Kajana, wilayani
Buhigwe mkoani Kigoma amepoteza maisha baada ya kulipukiwa na bomu
mwishoni mwa wiki.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma,
Kamishna Msaidizi James Manyama amesema;

“Mtoto huyo Abas Jeras, mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya
Msingi Lemba Kijiji cha Kasumo Kata ya Kajana alipatwa na mkasa huo
Agosti 28  mwaka huu baada ya kuokota bomu bila kujua na kuanza
kulichezea kisha bomu hilo kulipuka na kusababisha apoteze
maisha,”

Polisi inahusisha uwepo wa bomu hilo katika kijiji hicho kuwa huenda
lilikuwa eneo lililokuwa likitumiwa kama njia na makundi ya waasi
waliokuwa wakitoka nchi ya Burundi kwenda Kambi ya Wakimbizi ya
Mtabila, hivyo kudhaniwa kuwa huenda liliangushwa na watu hao.

“Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi wote wanaoishi vijiji
vinavyopakana na nchi ya Burundi kuwakataza watoto kuokota vitu na
kuvichezea ili kuepusha madhara kama yaliyotokea,”amesema.