*Amtaka mkandarasi kuhakikisha unakamilika kwa wakati
Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online-Kagera
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi,ameridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa soko la Bukoba Mjini,uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 18.9 hadi kukamilika kwake fedha inayojumuisha na ujenzi wa stendi ya mabasi.
Huku akimtaka mkandarasi wa ujenzi wa soko hilo, Nixxon Kissa, kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati uliopangwa ili wananchi waanzishe kunufaika nao.

Akizungumza Machi 26,2026 mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa soko hilo,ambao utekelezaji wake ulioanza Oktoba mwaka 2025, na kutarajiwa kukamilika Januari 2027,ukiwa umefikia asilimia 19, Kihongosi amepongeza juhudi zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanza utekelezaji wa soko hilo, uliotolewa ahadi zaidi ya miaka 10 bila ya utekelezaji.
“Nimpongeze mkandarasi anayejenga soko hili, ujenzi ni mzuri na umeendana na kiasi cha fedha kilichotolewa,hivyo itoshe kusema kuwa chama kilimeridhishwa”, amesema Kihongosi.
Pia amewataka baadhi ya viongozi wanaosimamia mradi wa soko hilo, akiwemo Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa huo,kuhakikisha wanatoa vipaumbele kwa wafanyabiashara awali waliokuwa wakifanya shughuli zao katika soko hilo, ambao walipisha ujenzi wa soko jipya, huku akitoa onyo kwa viongozi kuto hodhi maeneo katika soko hilo.
Sanjari na hayo, Kihongosi amewataka wananchi kuendelea kudumisha amani ya nchi na kutokubali kuhusika katika kuhamasisha uvunjifu wa amani.
Katika taarifa ya soko hilo, imeelezwa kuwa, soko la Bukoba Mjini litakuwa na vizimba 1848, maduka 132 ya hali ya kawaida na ya juu zaidi ya 30 pamoja na maegesho ya mgari.



More Stories
NMB ilivyosaidia Serikali kukusanya zaidi ya Sh trilioni 9.8
Serikali yaongeza nguvu kwa wachimbaji wadogo,yasisitiza usalama Migodini
REA imeleta mageuzi sekta ya nishati