December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mpigampicha Mbeya amvaa Dkt. Mwakyembe jimbo la Kyela

Esther Macha, TimesMajira Online, Kyela

MPIGAMPICHA maarufu Jijini Mbeya, Obadia Mwakibinga amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Kyela.

Mwakibinga amesema nia ya kuomba kuteuliwa ni kusaidiana na wananchi wa Kyela kuleta maendeleo. 

Aidha amesema changamoto zaJjimbo la Kyela ni pamoja afya, maji, miundo mbinu ya barabara maeneo ya vijijini ni changamoto kubwa. 

Akimkabidhi fomu ya kugombea Ubunge, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kyela, Lucas Nyanda amewataka wagombea kufuata  kanuni na taratibu za chama ikiwa  ni pamoja na kuacha tabia ya  kujipitisha kwa wapiga kura kabla ya kampeni kuanza.