April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mobetto aachia wimbo mpya ‘Ex wangu remix’

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva, Mwanamitindo na Mjasiriamali hapa nchini Hamisa Mobetto,ameachia ngoma mpya ijulikanyo ‘Ex wangu remix’.

Ndani ya video ya ngoma hiyo pia anaonekana mwanawe aliyezaa na msanii wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Wasafi Media Diamondplatnumz aitwaye dylandeetz.

Kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Mobetto amesema, “Nani ana mmiliki Ex wako?. ‘Exwangu remix’ nikiwa na Seneta Kilaka, Video & Audio zipo tayari kwenye Platforms zote za Muziki, gusa link kwenye BIO yangu Tukaenjoy Muziki Mzuriiikidogo,” aliandika Mobetto.

Miongoni mwa nyimbo ambazo Mobetto amefanya vizuri ni Madam Hero, Sawa, Sensema, Ginger Me, Boss, Tunaendana na nyinginezo.