April 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge wa Makete Festo Sanga akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani).

Mbunge Makete awaasa wabunge wa Bunge la 12

Na Joyce Kasiki,TimesMajira,Online

MBUNGE wa Makete Festo Sanga(CCM) amewaasa wabunge wenzake kufanya siasa za vitendo katika kuwaletea wananchi maendeleo badala ya siasa za mdomoni.

Sanga amesema hayo jana mkoani Dodoma katika viwanja vya Bunge wakati akiongea na TimesMajira ,amesema kuwa Bunge la sasa ni la kazi na siyo  la ndiyo mzee kama wengine wanavyodhani.

“Wote ni mashuhuda,Rais Dkt.John Magufuli amekuwa na ‘speed’ kubwa katika utendaji wake,na sisi wabunge tunatakiwa kwenda  na speed ya Rais ,

” Hatutakiwi kuwa na siasa za maneno,tunatakiwa kuzungumza pamoja na kutenda,wananchi wanatakiwa kupata maendeleo kupitia sisi wawakilishi wao.” Amesema Sanga na ameongeza kuwa

“Hilo siyo bunge la ndiyo mzee , siyo kitu kizuri kukaa bungeni  kama bubu ,lazima tufanye kazi kwa kasi kubwa .”

Akizungumzia kuhusu jimbo la Makete amesema,jimbo hilo linakabiliwa na changamoto kubwa ya barabara ya kutoka Makete kwenda Mbeya .

“Hilo ni miongoni mwa jambo nitakalolifanyia jitihada kuhakikisha tunapata barabara ya kiwango cha lami kutoka Makete kwenda Mbeya ili kurahisisha usafiri kwa wananchi.” Amesema Sanga

Pia amesema atashughulikia changamoto za zahanati ,Elimu,maji pamoja na michezo.

“Tuna changamoto ya zahanati,lakini ipo ambayo inahitaji kumaliziwa nitafanya hivyo,pia katika suala la Elimu tunatamani kutokomeza ‘zero’ katika jimbo letu hivyo tutaweka mikakati ya nini cha kufanya ili kulifanikisha.” Amesema