May 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Abbas Adam mmoja wa washiriki wa mashindano ya wazi ya TPC yanayoendelea kuchezwa katika viwanja vya kiwanda cha miwa cha TPC moshi Mkoani Kilimanjaro.

Mashindano ya wazi ya TPC yaendelea kutimua vumbi mkoani Kilimanjaro

Na Mwandishi wetu

WACHEZAJI wa ridhaa wa Mchezo wa Golf wameshiriki mashindano ya wazi ya TPC yanayoendelea kuchezwa  katika viwanja vya kiwanda cha miwa cha TPC moshi Mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza leo wakati wa kuanza kwa mashindano hayo Nahodha kwa klabu ya Golf  ya TPC,Jaffary Idd amesema Malengo ya mashindano hayo ni kukuza mchezo huo na kuongeza idadi ya wachezaji.

“Tunaendelea kukuza mchezo  hatua sio mbaya  tuna vijana wengi sana wanacheza,tunaamini baada ya muda mfupi tutakuwa na wachezaji wengi wazuri kwa maslaho ya Taifa,”amesema

Aidha  alisema programu ya watoto imekuwana tija na imekuwa kipaumbele na wanatarajia kuendesha mashindano makubwa ili kuendelea kutoa hamasa.

Kwa Upande wake Mchezaji namba moja wa Klabu hiyo,Ally Mcharo amesema matumaini yao makubwa ni kupata ushindi.

Mcharo ambaye kiwango chake cha uchezaji ni zaidi ya fimbo tano amesea baada ya kumaliza mashindano hayo anamatumaini makubwa ya Klabu kumpa fursa zaidi kimataifa .

Naye Mchezaji upande wa timu ya wanawake,Hadija Selemani wa Timu ya Golf Lugalo amesema mchezo ni mgumu ila anaamini watafanya vizuri.

Hadija ni miongoni mwa wachezaji 10 wa Lugalo walioshiriki mashindano hayo sambasamba na wachezaji wengine kutoka Arusha  Gymkhana ,Moshi na Kili Golf.

Mashindano hayo ya wazi ni ya siku mbili kwa wachezaji wa ridhaa na wakulipwa yanatarajia kuhitimishwa kesho jumapili  huu kwa wachezaji wa kulipa yanatarajia kuhitimishwa leo baada ya kuanza jana.