April 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Afisa wa Jeshi la Polisi mjini Gujarat akiwa amemdhibiti mmoja wahamiaji wafanyakazi wakati wa maandamano ya kushinikiza Serikali ya Gujarat kutoa vibali vya wao kurejea nyumbani wakati huu ambao Taifa la India linaendelea na utekelezaji wa agizo la zuio la kukaa ndani ili kuepuka kusambaza virusi vya corona. Wafanyakazi hao wanatokea mjini Surat,Ahmedabad uliopo zaidi ya kilomita 270. (Picha na AFP).

Matukio mbalimbali duniani (picha)

Afisa wa kijiji,Darth Vader akiwa amevalia mavazi maalum huku akiendesha boti ndogo iliyobeba bidhaa kwa ajili ya kusambaza kwa wanakijiji waliokumbwa na mafuriko eneo la Artex Compound lilopo Malabon, Metro mjini Manila, Ufilipino juzi. (Picha na REUTERS).
Upinde wa mvua ukionekana mara mbili karibu na mwanamke ambaye alikuwa ameshikilia mwamvuli huku akiuza vitafunwa katika kaunti ya Siaya nchini Kenya juzi. (Picha na REUTERS).
Watu wakishuhudia madhara yaliyotokea baada ya nyumba kuanguka kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi katika Mji wa Sanaa, Yemen. (Picha na REUTERS).
Mfanyabiashara Mohamed Mustafa Shahul Hamid (katikati) ambaye anafanya biashara ya nyama katika Soko la vyakula la Tekka nchini Singapore, na mwanae Nizamdeen, (38) wakijiandaa tayari kwa ajili ya kuuza nyama mubashara kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook juzi. Ubunifu huu unatwajwa kuwa na manufaa zaidi kwa wafanyabiashara wengi kipindi hiki cha corona. (Picha na GAVIN FOO/ST).
Baadhi ya ndege za Singapore Airlines, Scoot na SilkAir zikiwa katika moja ya maegesho ya karakana ya Alice Springs iliyopo Kaskazini mwa Australia zikisubiria siku ambayo virusi vya corona vitakoma ili kuweza kuanza safari za kimataifa. Ndani ya karakana hiyo jana zilikuwa ndege zaidi ya 25 na zinatarajiwa kuongezeka hadi kufikia 100. (Picha na ST).