Waziri Mkuu wa Somalia, Mohamed Hussein Roble amesema amesikitishwa na ghasia za usiku wa Jumapili iliyopita katika mji mkuu wa Mogadishu kati ya vyombo vya usalama vya serikali na vikosi vya upinzani.
Roble amesema,mazungumzo na kuelewana ndio njia pekee za kutatua mkwamo wao ambao umeendelea kuletataharuki kwa muda mrefu nchini humo.
Mapigano yaliripotiwa nyumbani kwa kiongozi wa chama cha upinzani cha Wadajir, Abdulrahman Abdishakur nanyumbani kwa Rais wa zamani, Hassan Sheikh Mohamud.
Rais huyo wa zamani ni miongoni mwa wale wanaopinga kuongezwa kwa muda wa Rais Mohamed Abdullahi Mohamed (Farmajo).

More Stories
Tanzania yaongeza nguvu ajenda ya Wanawake Duniani
Kapinga:Taka sifuri kukuza sekta ya viwanda
JWTZ ,Majeshi EAC yaimarisha ushirikiano