May 13, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kukamilika Kituo Cha afya Kasu kwaleta kicheko

‎Na Israel Mwaisaka, Nkasi

‎Wananchi wa kata ya Nkandasi wilayani Nkasi wamedai kukamilika kwa ujenzi wa Kituo Cha afya Kasu kumewaondolea adha kubwa ya kutafuta matibabu mbali na kuwa na uhakika WA afya zao.

‎Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya Wananchi hao wamedai kuwa wamekua na uhitaji wa muda mrefu wa kuwa na Kituo Cha afya katika kata hiyo na kuwa kitendo Cha Serikali kupeleka Fedha kwa ajiri ya ujenzi wa Kituo hicho Cha afya ni kitendo ambacho kimewafurahisha na Sasa huduma nyingi za kiafya zinapatikana hapo.

‎Sesilia Philbert mkazi wa Kijiji Cha Kasu alidai kuwa eneo hilo lina Watu wengi na huduma hiyo imekua ikifuatwa mbali na kuwa Sasa huduma nyingi za kiafya zimesogezwa karibu na kuwa jamii inapata huduma kwa wakati na kuwafanya kuwa na afya.

‎Amesema kuwa moja ya huduma ambazo zimekuwa zikitolewa katika Kituo hicho ni za uzazi na upasuaji  na kuwa kwa Sasa wasiwasi wa kupoteza uhai wa Mama au Mtoto wakati wa kujifungua umepungua sana kwa maana wengi wanahudumiwa kwa wakati na kuwa salama.

‎Adelina Gabriel mkazi wa Kijiji Cha Londokazi kwa upande wake amesema kuwa anampongeza Dkt,Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha upatikanaji wa Kituo hicho  cha afya na kuwa wahudumu wa Kituo hicho wamekua na weredi mkubwa na kuwa huduma wanazozipata ni nzuri na kwa wakati.

‎Amesema kuwa baadhi ya huduma zilikua ngumu kuzipata kulingana na foleni kubwa ya Wagonjwa katika vituo vya afya ya Namanyere, Sumbawanga na Chala na kuwa ni rahisi hata kupata vipimo na kujua afya tako na kuweza kuwai kuanza kupata matibabu kabla ya ugonjwa kukomaa.

‎Mganga Mkuu mfawidhi wa Kituo Cha afya Kasu George Japhet Hemed amekiri Kituo hicho kupokea Wagonjwa wengi wenye maradhi tofauti na kesi nyingi wanafanikiwa kiasi Cha wengi kupenda kupata huduma katika Kituo hicho .


‎Amesema kutokana na Imani kubwa waliyonayo  Wananchi juu ya huduma zitolewazo  katika Kituo hicho Cha afya,imepelekea Kituo hicho kuongoza katika makusanyo kupitia mfumo wa serikali mtandao wa kukusanya maduhuri hayo yaserikali.

‎ Hemed amebainisha huduma zinazotolewa katika kituo hicho ikiwemo huduma ya kliniki ya wajawazito,huduma ya kliniki ya watoto,huduma ya msamaha,huduma za dharura kwa wagonjwa,huduma ya vipimo vya maabara,huduma za rafiki kwa vijana,huduma kwa ajili ya ukatili wa kijinsia.

‎Ameongeza kuwa uwekezaji uliofanyika katika Kituo hicho Cha afya umeigharimu Serikali Zaidi ya Bil.1.3 ambapo uwekezaji huo umeleta chachu kwa jamii kwa kuweza kupatikana huduma bora za afya