May 27, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jeshi la Polisi kufanya marekebisho kanuni zake

Na Mwandishi Wetu

JESHI la Polisi nchini (TPF) limejipanga kuimarisha mradi wa utendajikazi katika kusimamia sheria ili kuzuia uhalifu pamoja na machafuko yanayoweza kutokea katika jamii.

Kwa mujinu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana imesema kuwa utekelezaji wa mradi huo utafanyika kwa lengo la kusimamia utawala na haki za binadamau nchini ili kutekeleza sheria kama maagizo ya Polisi yanavyoeleza.

Taarifa hiyo imesema kuwa mradi huo utafanyika katika maeneo ya Kanda ya Zanzibar, Kanda ya Kusini, Kanda ya Mashariki, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati, Kanda ya Magharibi na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa ya hivi karibuni imeonyesha kuwa kuna mambo mengi muhimu ambayo hayafuati sheria na kanuni,kutokwenda sawa kwa sheria zinazosimamia ujangili kwa Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii Dkt.Mussa Mussa alisema kuwa Jeshi la Polisi liko chini ya Mpango wa Mageuzi tangu 2006 chini ya hati yake ya mageuzi ya Mpango wa Marekebisho ya Jeshi la Polisi Tanzania (TPFRP) Mkakati wa Kati wa Muda wa 2010 /2011 hadi 2014/2015.

“Kazi ya Jeshi la Polisi si tu kutekeleza sheria lakini pia inafanya kazi na jamii kutatua changamoto zinazowaathiri na ndiyo maana kwa sasa tunafanya kazi katika kukagua baadhi ya maagizo ya Polisi,” alisema.

Dkt. Mussa aliongeza kuwa Programu ya Mabadiliko ya Polisi inakusudia kuunda kikosi kinachopatikana na kinacholenga kutoa huduma kwa uhuru na zinazokwendana na jamii katika kuhakikisha kuwa inatekeleza jukumu lake la msingi la kulinda raia.

Dkt.Mussa pia alishukuru msaada uliotolewa na wadau wengine kama vile Kituo cha Huduma za Sheria (LSF) kwa kukuza haki za binadamu na upatikanaji wa haki nchini Tanzania.

“Jeshi la Polisi linashirikiana na taasisi ambazo tunadhani tunaweza kufanyakazi kwa pamoja na msaada wa LSF kwa hafla za aina hii unathaminiwa sana na tunatumai inaendelea kufanya kazi na Jeshi la Polisi,” alisema.

Alisema kuwa TPF imepiga kusimamia mfumo wa demokrasia na wa kirafiki zaidi wa kuhakikisha amani na usalama endelevu vinapatikana nchini.

Alisema kuwa moja ya utekekezaji ni kurasimisha Dawati la Jinsia na watoto na TPF-Net, mfumo mzuri wa Sheria ya Uhalifu, kuboresha ufanisi na usawa wa shughuli za Polisi.