May 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkutano mkuu wa ALAT 2024; Waziri Mchengerwa atembelea banda la PSSSF

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma umeshiriki kwenye Mkutano Mkuu wa 38 wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa Tanzania (ALAT) uliofanyika jijini  Zanzibar na kupata fursa ya kuelimisha kupitia maonesho na uwasilishaji wa mada kwa wajumbe wa mkutano Mkuu.

Mkutano huo muhimu hujumuisha Wenyeviti wa Mikoa na Halmashauri zote nchini, Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa zote nchini, Mameya, na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya ALAT.

Meneja wa Ofisi ya Zanzibar wa PSSSF, Bi. Amina Kassim aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kuhusu maboresho ya kidijitali yaliyofanywa na PSSSF ili kuboresha huduma kwa wateja ikiwemo kuhusu mfumo mpya wa kupokea madai ya mafao mtandaoni na usajili wa wanachama mtandaoni.

Aidha aliwaomba waendelee kutoa ushirkiano ili kutatua changamoto za kiutendaji kwa wakati.

Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa na kufungwa na Waziri wa Nchi Ofisi yanRais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohamed.

Mkutano Mkuu umehudhuriwa na  wajumbe na taasisi wadhamini takribani 450.