May 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Muandaaji wa shindano la Bongo Star Searh (BSS), Ritha Paulsen, 'Madam Ritha', (wa kwanza kulia), akiwatambulisha maji wapya Christian Bella na Omary Nyemo,'Ommy Dimpoz', mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani.

Christian Bella, Ommy Dimpoz majaji wapya BSS 2020

Na Mwandishi Wetu, Times Majira Online

SHINDANO la kusaka vipaji la Bongo Star Search (BSS), msimu mpya wa 2020, wamewatambulisha majaji wapya wawili kwenye shindano hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati wa kutangaza majaji, muandaaji wa shindano hilo, Ritha Paulsen, ‘Madam Ritha’ amesema, mwaka huu wamefanya mabadiliko katika safu ya majaji.

“Napenda kuwataarifu kuwa msimu wa 11 majaji watakuwa ni Chief jaji Madam Ritha, Johakim Kimario, ‘Master J’, Christian Bella, Omary Nyemo,’Ommy Dimpoz’, na mshehereshaji wa kipindi atakuwa Idris Sultan”.

Hata hivyo alisema, usahili utaanza kwenye mkoa wa Mbeya Septemba 19 mwak huu katika ukumbi wa Dhamira na Point Zone Resort, kwa Mkoa wa Arusha utafanyika Septemba 26 na Mwanza Octoba 3 kwenye Hotel ya Isamilo, Oktoba 10 itakuwa Mkoani Dodoma ukumbi wa Royal na Dar es Salaam itakuwa Octoba 17, 18 ambapo itafanyika Makumbusho ya Taifa.