May 27, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Harmonize kurudisha fadhila kwa jamii

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa Kondegangs, Rajabu Abdul maarufu kama ‘Harmonize’ ameamua kuandaa Tamasha maalum lujulikanalo kama (One Love Concert), litakalofanyika siku ya Jumapili Machi 20 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Akiweka wazi hilo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram, Harmonize amesema lengo la Tamasha hilo kurudisha fadhila kwa jamii kwa kufurahi na Walemavu, Watoto Yatima, Wakina mama Wajane na watu wengine wasiojiweza.

“Nimeamua kuitumia siku hii kutengeneza furaha kwenye mioyo ya watu wengine angalau kwa siku moja. Bila shaka mimi na wewe tutajumuika pamoja Tarehe 20/03/2022 siku ya Jumapili pale Mlimani City, Dar es Salaam kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 12: jioni.

“Tamasha hili litahusisha, Walemavu, Watoto Yatima, Wakina mama Wajane na Watu wengine wasiojiweza. Lengo ni kutengeneza furaha ya pamoja, hivyo tutapata chakula cha mchana na tutaimba nyimbo zote.

“Nachukua fursa hii pia kutoa wito kwa Kondegang FC wote pamoja na yeyote ambae yupo tayari kutengeneza faraja katika makundi husika niliyo yataja hapo juu, basi unaweza kuchangia vitu vifuatavyo Chakula cha aina yeyote,” amesema Harmonize.