May 4, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Diamond: Wanawake wanataka pesa sio mapenzi

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira

Nyota wa muziki hapa nchini na Bosi wa Wasafi Media, Diamondplatnumz amesema kila msichana anahitaji pesa sio mapenzi hivyo ni vyema wanaume wakatafuta hela.

Akitoa ujumbe huo kupitia ig stori yake, Diamond amesema mwanamke mfanyie mambo milioni ila ukipata shida kidogo ya kifedha utajua balaa lake.

“Kuhusu pesa na mapenzi, “Kila msichana anataka
Pesa kutoka kwako na sio Mapenzi yako ya Kweli ya kijinga.

“Mfanyie mambo milioni ila ukipata shida kidogo ya kifedha na uchelewe kufanya moja ya mambo ambayo anataka, hapo utajua tabia yake halisi. Ndugu zangu Tutafteni ela!,” amesema Diamond.