Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online,Morogoro
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, Waziri Kombo amewataka wawekezaji kujitokeza kuja kuwekeza katika wilaya hiyo ambayo ardhi yake haina migogoro
Kombo ameyasema hayo mwishoni mww wiki alipohudhuria ufungaji wa maonesho ya Nanenane ya mwaka 2026 Kanda ya Mashariki katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Manispaa ya Morogoro
Amesema wawekezaji ambao wanataka kuwekeza katika wilaya hiyo wanatakiwa kufika katika ofisi za halmashauri hiyo zilizopo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kupata baraka zote kwa viongozi.

Aidha, amesema katika bajeti mpya ya mwaka 2026/27 halmashauri imetenga maeneo mapya matano kwa ajili ya uwekezaji
” Tunawakaribisha wawekezaji wote kuja kuwekeza katika maeneo yaliyotengwa na halmashauri yetu kwa kufuata utaratibu uliowekwa na ili kuepuka migogoro,” amesema Kombo
Halmashauri ya Manispaa ya Mkuranga katika kuhakikisha kuwa wananchi pamoja na wadau wengine wa shughuli za Kilimo, Mifugo na Uvuvi wanapata fursa ya kujifunza na kupata maarifa ili iwe chachu ya kuongeza tija katika uzalishaji imeendelea kuongeza kutenga maeneo ya uwekezaji,” amesema
Ameyataja maeneo mapya yaliyotengwa kwa uwekezaji katika bajeti mpya kuwa ni pamoja na Kazole, Kimanzichana, Mbezi,Nyamato na Msolwa.

Akizungumzia faida za kushiriki maonesho ya nanenane amesema yamewawezesha kutangaza bidhaa zao sà mbamba na kutangaza mambo ambayo halmashauri inafanya
Awali wakati akikagua katika Banda la Halmashauri hiyo Kombo amewasihi wajasiriamali kuhakikisha wanakuwa na nyenzo muhimu za kuhakikisha mbali na kuuza bidhaa zao lakini pia wanatumia jukwaa hilo kuwapatia uelewa wananchi.
Hata hivyo banda hilo pia lilitembelewa na madiwani wa Kata zote za Mkuranga na Wakuu wa Idara mbalimbali kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali na bidhaa zinazozalisha.
k

More Stories
Awamu ya pili ya uvutaji nyaya Chalinze–Dodoma kuanza kesho
Rais Samia atoa msukumo wa Masoko ya Mazao
Mainstream Group yapata Tuzo mbili TEHAMA Awards 2026