March 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DC Mjema: Mafao si ya kuolea watoto wadogo

Na Bryceson Mathias,Timesmajira Online, Arusha

MKUU wa Wilaya Arusha Mjini, Sophia Mjema amewataka Wastaafu zaidi ya 400 mkoani Aruasha, wasitumie mafao yao watakayopata kwa ajili ya kuoa watoto wadogo na kuolewa na vijana wadoogo kwa sababu watakufa haraka watakapowapa kihoro.

Mjema ameyasema hayo wakati akifungua semina ya elimu ya wastaafu watarajiwa zaidi ya 400 mkoani Arusha kwenye semina ya uwekezaji kwa maisha endelevu, baada ya kustaafu iliyoandaliwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa umma iliyofanyika Lush Gardern na kufadhiliwa na taasisi tisa za kibenki.

Akifungua Semina hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amesema wastaafu akinababa anataka wakipata mafao wasiende kuoa wasichana wadogo wadogo na akinamama nao wasiende kuwaweka ndani vijana wadogo kwa kuwa wakilizwa mtakufa haraka.

“Akinababa wastaafu andaeni maisha yenu vizuri na kujikinga na maradhi, msikimbilie kununua (kuoa) magari madogo ‘Ditto’ wasichana wadogo) na akinamama wastaafu msikimbilie kuwaweka ndani vijana wadogo ‘Vi-Mask’, maana watakapowakimbia, fedha zikiisha mtakufa haraka kwa kihoro,” amesema.

Mjema amewataka akinamama wastaafu fedha watakazopata ni zao si za wajukuu wao, wajukuu ni wa watoto wao na kama wakienda kuwatembelea watoto wao, wasiende kwao kuwavuruga; “Ukienda kwao kapange hotelini, ili kuondokana na kwamba unawasaidia kupika au kufagia nyumba,” amesema.