April 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chongolo RC mpya Songwe

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuhamisha Dr. Batilda Salha Burian kutoka Mkoa wa Tabora kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga akichukua nafasi ya Waziri Kindamba.

Rais Samia pia amemteua aliyekuwa DC wa Misungwi Paul Chacha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora akichukua nafasi ya Dr. Batilda.