August 24, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Burudani zapamba utambulisho wa ‘Fanta Berry’ nchini

Burudani zapamba utambulisho wa ‘Fanta Berry’ nchini

Na Mwandishi Wetu,Timesmajira Online

BURUDANI ya muziki imewapagawisha mashabiki baada ya Chapa ya Fanta kutambulisha ladha mpya ya Fanta Berry nchini, ikiwa ni hatua ya kuongeza chaguo kwa watumiaji wanaopenda vinywaji vyenye ladha tofauti za matunda.

Ladha hiyo mpya, ambayo inalenga zaidi kuwafikia vijana, imekuja wakati muziki, mitindo, dansi na ubunifu wa maudhui vikiendelea kuwa sehemu kubwa ya maisha na burudani kwa vijana nchini.

Fanta Berry pia imehusishwa na nguvu ya muziki wa Singeli, ambao umeendelea kukua na kujenga nafasi yake miongoni mwa vijana wa Tanzania.

Akizungumza kuhusu ujio wa ladha hiyo hivi karibuni,  Meneja Mwandamizi wa Masoko wa Coca-Cola Tanzania,  Kabula Nshimo amesema Fanta Berry inalenga kuongeza chaguo kwa Watanzania kulingana na ladha na mapendeleo yao.

“Tunafurahi kuleta chaguo jipya kwa Watanzania kupitia Fanta Berry. Tunaendelea kuangalia ladha na mapendeleo ya watumiaji wetu na kuwapa chaguo mbalimbali za vinywaji wanavyoweza kufurahia katika nyakati tofauti,” amesema Nshimo.

Uzinduzi wa Fanta Berry utaambatana na kampeni ya “Kipapli”, ambayo itawafikia vijana kupitia muziki, dansi, mitindo, watengeneza maudhui na shughuli mbalimbali za burudani katika vyuo vikuu na maeneo yenye mikusanyiko ya watu jijini Dar es Salaam.

Kupitia kampeni hiyo, vijana watapata nafasi ya kuonja Fanta Berry, kushiriki katika burudani na shughuli mbalimbali zitakazowapa nafasi ya kuonesha vipaji na ubunifu wao.

Kama sehemu ya kutambulisha ladha hiyo kwa Watanzania, Coca-Cola Kwanza iliendesha msafara ulioanzia katika kiwanda chake cha Mikocheni na kupita maeneo ya Ubungo, Mabibo, Buguruni na Temeke, kabla ya kuhitimishwa Mbagala.

Katika maeneo hayo, wananchi walipata nafasi ya kuonja ladha mpya ya Fanta Berry kwa mara ya kwanza pamoja na kushiriki katika muziki, dansi na burudani nyingine.

Mbali na kutambulisha ladha mpya, kampeni hiyo inatarajiwa pia kutoa nafasi kwa vijana kuonesha ubunifu wao kupitia utengenezaji wa maudhui na kutumia majukwaa ya kidijitali kufikia watu wengi zaidi.

David Chait, Meneja Mkuu wa Coca-Cola Kwanza Ltd, amesema kuongezeka kwa chaguo la bidhaa kunalenga kukidhi mapendeleo tofauti ya Watanzania.

“Watanzania wana ladha na mapendeleo tofauti. Ndiyo maana tunaendelea kuongeza chaguo la bidhaa zetu ili kila mmoja aweze kupata kinywaji anachokipenda na kukifurahia katika nyakati mbalimbali,” amesema Chait.