April 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BRELA yaja na wiki ya suluhisha kutatua migogoro ya makampuni

Na Iddy Lugendo, Timesmajira online

BRELA yaja na wiki ya suluhisha “WIKI YA SULUHISHA NA BRELA” kwa ajili ya kusikiliza malalamiko, changamoto mbalimbali kutoka kwa wanahisa, wakurugenzi wa makampuni ambazo wamekuwa wakikutana nazo na kuwakutanisha kwaajili ya kujadili kwa pamoja ili makampuni yaweze kuendeshwa vizuri na kufanya biashara katika mazingira mazuri.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 13, 2022 jijini Dar er salaam kaimu mkurugenzi wa idara ya makupuni na majina ya biashara (BRELA) Meinrad Rweyemamu amesema lengo la wiki ya suluhisha na Brela kumekuwa na wamiliki wa makampuni kutaifishwa pamoja na kuwepo kwa migogoro katika makampuni yao, hiyo kupitia wiki hii wataweza kupata suluhisho la migogoro inayowakumba.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Makampuni na majina ya Biashara (BRELA), Meinrad Rweyemamu akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 13, 2022 mara baada ya kuzindua WIKI YA SURUHISHA NA BRELA yenye lengo la kutatua migogoro ya makampuni nchini.

“Kwenye Kampuni mwenye hisa hutokea amefariki huku ndugu hawafahamu kinachoendelea kwenye kampuni, hawafahamu zile hisa za marehemu ni mali kama mali zingine ambazo zinagawiwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Njoo katika wiki hii tutakuwa pamoja, tutaangalia haki yako ni ipi”. Amesema Rweyemamu

Aidha amesema watakaa na wamiliki pamoja na wahusika kujadiliana na kupeana elimu mwisho wa siku kila mtu apate haki yake na kuondokana na migogoro ambayo imekuwa ikitokea kwenye makampuni mbalimbali.

Hivyo wiki ya suluhisha na Brela inayoanza leo Juni 13, 2022 na kufikia tamati siku ya jumapili Juni 19,2022 wenye makampuni wametakiwa kufika eneo husika ambalo ni Makumbusho ya Taifa Posta Jijini Dar es Salaam ili waweze kutatuliwa changamoto zao.