May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba

BREAKING NEWS: Wanne wanaswa na dawa za kulevya Shinyanga

Na Suleiman Abeid, Shinyanga

WATU wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroin zilizokuwa zimefichwa ndani ya nyumba ya mmoja wa watuhumiwa hao.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba amewataja watuhumiwa waliokamatwa ni Hassan Ibrahim (22), Abdalah Hemed (23), Chiku Tungu (57) wote wakazi wa Majengo Manispaa ya Shinyanga na Juma Omary (26) mkazi wa kata ya Ngokolo Shinyanga.

Kamanda Magiligimba amesema watuhumiwa hao walikamatwa Aprili 19, saa 6.00 mchana katika mtaa wa Majengo kata ya Kambarage baada ya Polisi kupokea taarifa za kiintelejensia.

“Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo, Polisi walikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa Chiku Tungu na kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa ndani ya uzio wa nyumba hiyo na kukutwa na dawa hizo ambazo ni pinchi 08 za heroin, rizla, kitezo, kigae na kisu kimoja na tayari watuhumiwa wote tunaendelea kuwahoji na baada ya kukamilisha mahojiano tutawafikisha mahakamani kujibu shitaka linalowakabili,” amesema Magiligimba.