January 19, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

BREAKING NEWS; Rais Samia awalilia askari waliouawa Dar

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira,Online, Dar
RAIS Samia Suluhu Hassan, ametoa salamu za pole kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, Inspekta Generali wa Polisi, familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia vifo vya askari watatu wa Jeshi la Polisi na askari mmoja wa kampuni ya ulinzi ya SGA vilivyotokea jana Agosti, Jijini Dar es Salaam.

Rais Samia amewataka Watanzania kuendelea kuwa watulivu wakati huu ambapo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama vikiendelea na uchunguzi wa tukio hilo la kihalifu lililotokea katika makutano ya Barabara ya Kenyatta na Kinondoni.

Aidha, Rais Samia amewaombea majeruhi wapone haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao.

Pia Rais amemuomba Mwenyezi Mungu azipumzishe roho za Marehemu Mahali pema Peponi, Amina.