December 30, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BREAKING: Mbunge wa Konde afariki, Bunge laahirishwa

Na Joyce Kasiki, TimesMajira Online, Dodoma

MBUNGE wa Konde Khatib Said Haji (ACT-Wazalendo) amefariki alfajiri ya leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Akitoa taarifa leo Bungeni jijini Dodoma,Naibu Spika Dkt.Tulia Ackson amesema mwili wa mbunge huyo utazikwa leo saa kumi jioni visiwani Zanzibar.

Kufutia kifo cha Mbunge huyo Bunge limeahirishwa hadi kesho saa tatu asubuhi.