Fresha Kinasa TimesMajira Online Mara.
MBUNGE anayemaliza muda wake wa Jimbo la Bunda Boniphace Mwita amerejesha rasmi fomu aliyochukua ya kuwania kutetea kiti chake kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Mwita, amerejesha fomu hiyo Julai Mosi 2025 kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Bunda Evodia Edward, Ambapo aliichukua Juni 28, 2025.
Aidha, Mwita ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Hassan kwa fedha nyingi za maendeleo alizotoa ambazo zimeleta maendeleo katika sekta mbalimbali.
Huku pia akisema, shauku yake ni kuendelea kuwatumikia Wananchi waJimbo hilo iwapo atapata ridhaa ya kuteuliwa kugombea na kushinda nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo.

More Stories
Mwenge waweka jiwe la msingi madarasa matatu Tunduma
Bunge lipo tayari kushirikiana na Mabunge mengine
TADB yatoa tuzo kwa wanafunzi 13 SUA