March 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bondia Mcgregor, Poirter kuzichapa kesho

LAS VEGAS, Marekani

BONDIA anaetajwa kuongoza listi ya wanamichezo

wanaovuta mkwanja mrefu zaidi duniani,Conor Mcgregor

atashuka ulingoni kesho jumapili kuzichapa na Dustin

Poirterkatika pambano la marejeano litakalofanyika Las

Vegas.

Hiyo ni katika pambano la UFC 264, likiwa ni pambano la

tatu kuwakutanisha miamba hiyo ya Mixed Martial Arts

[MMA] duniani.

Mara ya kwanza miamba hiyo ilikutana katika UFC 178,

pambano lililofanyika Septemba 2014 mjini Las Vegas,

Nevada Marekani ambapo CONOR, alishinda.

Mara ya pili walikutana Januari mwaka huu, katika UFC

257, pambano lililopigwa umoja wa falme za kiarabu,

mjini Abu dhabi, Poirter alishinda.

Kwa sasa Poirter ndie namba moja kwenye UFC lightweight

wakati Conor ambaye ni bingwa wa zamani wa UFC uzani wa

featherweight na Lightweight, akishika nafasi ya tano

kwenye uzani huo.