Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amekutana kwa mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia Cecep Herawan katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Pamoja na Mambo mengine, mazungumzo ya viongozi hao yamejikita katika kujadili masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Indonesia katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara na uwekezaji, kilimo, afya, elimu na nishati.

Balozi Shelukindo amemhakikishia Katibu Mkuu huyo ushirikiano wa dhati katika kuendelea kuimarisha uhusiano wa muda mrefu na na Indonesia.
Aidha, amemueleza kwamba mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ni mazuri na salama na kuwasihi wawekezaji kutoka Indonesia kuchangamkia fursa zilizopo.

Naye, Herawan amepongeza uhusiano imara uliopo baina ya serikali hizi mbili (Tanzania na Indonesia) na kuongeza kuwa Indonesia itaendelea kushirikina na Tanzania katika sekta mbalimbali kwa maslahi ya nchi zote mbili.

More Stories
MiXX Yakabidhi Zawadi kwa Washindi wa Kampeni ya Kombe la Dunia
Mwenge wazindua jengo lenye thamani ya bil 3.4
Mavunde kuwa mgeni rasmi LCCF 2026